
MSANII mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ amesema kuwa mpaka sasa hakumbuki idadi kamili za kolabo alizowahi kuzifanya.
Akizungumza kwenye kipindi cha +255 kinachorushwa na global radio, Jide alisema muda mwingine hadi apitie mafaili yake ndiyo anatambua kolabo alizozifanya.
“Tangu nilivyoanza muziki nimefanya kolabo nyingi sana na wasanii tofauti tofauti, kuna zingine hata sizikumbuki, kuna muda mwingine hadi nirejea kwenye mafaili yangu ya listi ambazo nimewahi kufanya ndiyo natambua,” alisema Lady Jay DeeHata hivyo, msanii huyo alisema nyimbo zote ambazo wasanii wanaompelekea huwa tayari anakuwa amekwishazipenda ndiyo maana anakubali kushirikiana nao.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx