Wachezaji Simba, Benchi la Ufundi Watua Bungeni
KIKOSI cha Klabu ya Simba leo Februari 3, 2021, baada ya kutinga makao makuu ya nchi, Dodoma, kimepata fursa ya kuingia ndani ya Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez, na Msemaji wa Klabu, Haji Manara.
Miongoni mwa wachezaji walitinga bungeni ni pamoja na Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Shomari Kapombe, Clatous Chama, na Mohamed Hussein.
Wengine ni Kenedy Juma, Hassan Dilunga, Ibrahim Ame, Beno Kakolanya, Aishi Manula, Pascal Wawa, Mzamiru Yassini, na Luis Miquissone.
Benchi la ufundi lilikuwa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, na kocha msaidizi, Seleman Matola.
Wengine ni Mratibu wa Klabu, Abbas Seleman, na Ofisa Habari wa Simba Haji Manara.