×

JPM: Mumeo Aliyefukuzwa Akatafute Kazi Nyingine – Video

RAIS John Magufuli, amemshauri mwanamke aliyedai kuwa mume wake alikuwa ni askari magereza na alifukuzwa kazi baada ya kusingiziwa kwamba aliwapelekea wafungwa simu, atafute kazi nyingine si lazima awe askari magereza.

 

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 4, 2021, mara baada ya kuzindua nyumba 24 za askari wa Gereza Kuu LA Isanga jijini Dodoma, ambako kina mama walijitokeza wakimuomba asikilize shida zao na awasaidie.

 

 

“Magereza yetu tunatakiwa tujenge nidhamu.  Sasa, akifukuzwa si akatafute shughuli nyingine huyo mume wako?  Kwani lazima aliambiwa atakaa tu kwenye magereza na yeye amesingiziwa kosa la kupeleka simu nne kwa wafungwa?” alisema Magufuli.

 

 “Hizi shida zote najua kila mmoja ana shida yake, lakini nina Madiwani, nina Ma-DC, Mwenyekiti wa Kijiji, Mbunge, RC hadi Waziri , wote mmeshindwa kuwauliza, mnataka nianze kila mmoja, huyu Mume wake alifukuzwa kazi nianze kujadili kwamba hakuingiza simu nne kwa Wafungwa.

 

“Wewe Diwani wako ameuza maeneo yako, yote haya, hata ungekuwa wewe Mama yangu, ni sawa umenichagua, shida za hapa kila mmoja wenu hapa nitaweza kuzitatua kwa Saa hii, Dakika moja na niujue ukweli uko wapi?, mna Mbunge unless awe hawajibiki, hii ndio kazi ya Mbunge.

 

 

Awali Magufuli, alimshauri mwanamke huyo kuonana na Mkuu wa Magereza: “Wewe mama mume wako alifukuzwa, mambo ya jeshi yana sheria zake, mwone Mkuu wa Magereza lakini mimi nitajua ukweli uko wapi wakati nafahamu kweli kuna askari Magereza siyo waaminifu wanawapelekea simu wafungwa na wengine hadi gongo na bangi.”

 

Leave a Comment