
MBUNGE wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, amewasihi wabunge wote kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, katika kutekeleza yale aliyopanga kuyafanya kwa miaka mitano (2020-2025) ili kuboresha maisha ya Watanzania na kuinua uchumi wa taifa.
Shigongo amesema hayo wakati akichangia Bungeni hotuba za Rais Magufuli alizozitoa wakati wa kufunga Bunge la 11 na wakati wa kufungua Bunge 12.