
STAA mwanamuziki Mmarekani, TikTok aka Dazhariaa Quint Noyes amefariki katika umri wa miaka 18 kwa kujiua Jumatatu wiki hii.
Nyota huyo aliyaandika yote hayo mtandaoni akisema: “Najua yanawakera nyote, lakini huu ndiyo mwisho wangu.l”

Dazhariaa aliyekuwa akitumia jina la Bxbygirlldee, alikuwa na wafuasi zaidi ya milioni moja katika TikTok na zaidi ya wafuasi 100,000 wa Instagram.
Wazazi wake walisikitishwa na uamuzi wake wa kujitoa maisha yake.


