The House of Favourite Newspapers

Ebitoke Hataki Mimba Kabla ya Ndoa

0

MSANII wa vichekesho Bongo, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ kwa mara ya kwanza amesema kuwa hajawahi kubeba ujauzito katika maisha yake ila anashangaa kwa nini watu waliamua kumuibulia hiyo skendo.

 

Akipiga stori mbili tatu na Mikito Nusunusu, Ebitoke amesema kuwa kuna kipindi watu walimzushia kuwa ana ujauzito jambo ambalo sio kweli kwa sababu katika maisha yake hajawahi kubeba mimba na wala hatarajii kuja kuwa na ujauzito kabla ya ndoa.

 

“Kuna kipindi watu walizusha kuwa nina mimba mara ghafla wakasema nimetoa, sio kweli jamani huo ulikuwa ni uzushi tu mimi sijawahi kubeba mimba kabisa na namuomba Mungu hata nikibeba iwe ni ndani ya ndoa kwa sababu hiyo ndio furaha ya kila mwanamke,” alisema Ebitoke.

STORI:MEMORISE RICHARD, RISASI

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply