
Coca-Cola Kwanza Ltd, ambayo ni kampuni tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa leo imetangaza kuzindua msimu mpya wa kampeni ya Mwanamke shujaa kwa lengo la kusherehekea michango na juhudi za wanawake wa Tanzania wakati huu wa kuelekea kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.
Kampeni hiyo, ambayo inatafsiriwa kuwa “Mwanamke shujaa”, inakusudia kutambua juhudi za Wanawake, kutoa fursa kwa Wanawake kuhamasishana, kujijengea mitandao, kujenga ujasiri na kubadilishana uzoefu kwa lengo la kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu, kulingana na kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Pia inalenga kusisitiza juhudi za Coca-Cola Kwanza katika uwezeshaji wanawake.
Kampeni hii pia itaweza kutambua juhudi za wanawake kutoka sekta mbali mbali katika jamii na kuwakumbusha juu ya kujiamini, kujithamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao.
Siku ya Kimataifa ya wanawake Duniani kwa 2021 inazingatia Wanawake katika uongozi na Coca-Cola kwanza kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wanawake imeamua kuzindua tuzo za “Excellence in Leadership Awards” ” katika sekta 10 tofauti kwa wanawake kwenye nafasi za uongozi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeini hiyo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Mauzo Coca-Cola Kwanza Josephine Msalilwa alisema nia ya kampeni pamoja na utoaji wa tuzo ni kusherehekea, kutambua na kuhamasisha wanawake kutoka sekta tofauti ambazo wanaweza.
“Kuhusu kampeini hii ni kusherehekea mafanikio ya wanawake pamoja na kuwahamasisha kwamba wao pia, wanaweza kufikia malengo yao na kupata mafanikio makubwa,” alisema Bi Msalilwa.
Msalilwa ameongeza, Watanzania wanaamini ni jukumu letu kuleta mabadiliko endelevu katika sekta tofauti ambazo wanawake wa Tanzania hufanya kazi kwa hivyo kuanzishwa kwa kampeni ya Mwanamke shujaa pamoja na utoaji wa tuzo inakusudia kukuza michango na kudhamini juhudi za wanawake kwenye jamii yetu.
“Tayari nimekutana na wanawake wenye hamasa na malengo mazuri hapa nchini Tanzania, ambao wameamua kuvunja vizuizi na kufikia mafanikio yao,” aliongeza.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni hiyo Yvette Gadi alisema, Kampeni ya Mwanamke shujaa inaungana na kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Mwanamke Duniani ya 65 ya Tume ya Umoja wa Mataifa juu ya Hadhi ya Wanawake;
“Ushiriki kamili wa wanawake kwenye kufanya maamuzi, na pia kuondoa vurugu, kwa kufanikisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote”.
Kampeni ya Usawa, ambayo inatoa haki ya wanawake kwenye kufanya maamuzi katika maeneo mbali mbali ya maisha yao.
Yvette aliongeza kuwa kampeni hiyo itakuwa ya muda wa wiki tatu na zaidi itakuwa ni ushirikiano kwa vyombo vya habari huku ikijumuisha wanawake katika kipindi vya moja kwa moja kupitia Televisheni, vipindi vya maandishi, vipindi vya mtu mmoja mmoja kwa njia ya mtandao, vipindi vya moja kwa moja vya maswali na Majibu kutoka kwa wanawake katika uongozi kwa wanawake vijana mashule pamoja na sherehe kubwa ya kufunga ambayo itakuwa ni usiku wa Excellence in leadership Awards.
Kwa upande wake, Sarah Pima ambaye ndio jaji mkuu wa kampeini hiyo alisema, lengo la kampeini hii ni kuthamini ubora wa wanawake kwenye nafasi za uongozi kwenye sekta mbali mbali pamoja na kuhamasisha wanawake wenzao kujifunza na kufanya vizuri kwenye majukumu yao.
Aliongeza kuwa kwa mwaka huu tumepanga kuwapa tuzo wanawake 10 bora katika sekta tofauti ambazo ni – Tuzo za Uongozi wa Elimu, Tuzo za Uongozi wa Michezo, Tuzo za Uongozi wa Biashara na Ujasiriamali, Tuzo za Uongozi wa Sekta ya Afya, Sayansi na Teknolojia, Tuzo za uongozi kwenye sekta ya Utalii,Tuzo za uongozi kwenye jamii na utamaduni, Tuzo za uongozi wa Vyombo vya Habari, Tuzo za uongozi wa Burudani na Tuzo za uongozi wa Biashara ya Kilimo
Coca-Cola Kwanza ltd imekuwa ikishiriki kwenye miradi mingi yenye uwesheshaji kwa wanawake ambayo ni pamoja na mradi wa 5by20, ambao ni mradi wa kimataifa wa Coca-Cola kutoa msaada wa kiuchumi kwa wanawake milioni 5 kuendesha biashara zao katika nchi zinazoendelea ifikapo 2020.
Coca-Cola Kwanza hadi sasa imeweza kutoa mafunzo (Biashara na Ujasiriamali), vifaa (Msaada wa Nyenzo) na pamoja na kujenga mtandao zaidi kwa wanawake wa Tanzania 50,000 kupitia mpango wa 5by20 ulioanzishwa na Mfumo wa Coca-Cola.
Coca-Cola Kwanza imekuwa na kipaumbele cha kurundisha baadhi ya faida kwa jamii kupitia ushirikiano na wadau wake.