×

Mwigulu: Wanaozusha Vifo Wakamatwe

 

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwachukulia hatua Watu wanaosambaza taarifa za uongo kuhusu Afya za wengine.

 

 

Dkt. Nchemba amesema kumekuwepo wa uvumi mwingi mitandaoni kuhusu hali za Afya za watu mbalimbali wakati kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandao kinazuia watu kutoa taarifa za uongo.

 

Amesema tabia ya kuzushiana ni kukosa utu, ni kuathiri maisha binafsi ya mtu, familia yake na kusababisha taharuki kwenye Jamii. Amewataka Wananchi kuacha tabia hiyo mara moja.

 

Mwigulu ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram;

Taifa lipo kwenye Msiba wa viongozi wetu ambao wametangulia mbele ya haki kwa Mapenzi yake Mungu, Kumetokea tabia mbaya ya kuzushiana, (Na fulani anaumwa, na fulani naye anaumwa.

 

Mara nasikia fulani amekufa na fulani naye amekufa), Huku ni kukosa UTU, ni kuathiri maisha Binafsi ya mtu, Familia yake na kusababisha TAHARUKI kwenye Jamii. Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao kinazuia watu kutoa taarifa za uongo.

 

Nimeelekeza vyombo vyote husika kuchukua hatua bila kusubiri mtu binafsi akalalamike.Nani amekupa kazi ya kufuatilia afya za wengine na kuwa msemaji wa hali zao?
TUACHE TABIA HII MARA MOJA

Leave a Comment