
ALIYEKUWA kuwa mbunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata, ameandika kuwa alidhani yeye ni jasiri, baada ya kumpoteza mume wake Dkt.Servacius Likwelile, aliyefariki dunia hii leo Jumamosi, Februari 20, 2021, baada ya kuugua ghafla.
Vicky Kamata, ameyaandika hayo hii leo kupitia akunti yake ya mtandao wa Instagram. “Nilidhani mimi ni jasiri, lakini kwa hili kumbe mimi si lolote, Mungu mbona umeniacha?” ameandika Vicky Kamata.
Dkt. Servacius Beda Likwelile, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na pia aliwahi kuwa Mhadhiri Idara ya Uchumi na Ndaki ya Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.