×

JPM Azindua Jitegemee House “Ufisadi Uliota Mizizi” – Video

 

Rais Magufuli amezindua Jengo la Jitegemee (Jitegemee House) na Studio za Channel Ten Plus, Radio Magic FM na Radio Classic FM ambapo akiwa kwenye Studio za Channel Ten amechagua na kupigiwa wimbo wa Baba wa Stamina ft Prof. Jay na One Six “huu wimbo una meseji.”

 

 

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Magufuli amesema; “Ufisadi ulikuwa uliota miziz, mpaka mali za chama zilikuwa zimeshaanza kuchukuliwa na watu. Nilipomteua Dkt. Bashiru kuwa Katibu Mkuu wa CCM akaanza kufuatilia wakasema ni CUF na mimi nikasema nataka CUF wa namna hii ndani ya CCM.”  

Aidha, Magufuli amewapongenza wafanyakazi wa Africa Media Group Limited ambayo ni Kampuni Tanzu ya Uhuru Media zinazomilikiwa na CCM kwa kuchapa kazi vizuri huku na wao wakimshukuru kwa kuboresha mazingira yao ya kazi kwa kuwajengea studio za kisasa na kuwanunulia vifaa vya kisasa vya kurushia matangazo.

 

FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA

Leave a Comment