
MSANII wa vichekesho ‘Uncle Zumo’ leo Februari 26, akiwa kwenye shoo ya Bongo 255, inayoruka kupitia Radio namba moja ya mtandaoni +255 Global Radio, amefunguka kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ya familia na tasnia ya uigizaji.
Alipoulizwa kuhusu kuongeza mke wa pili Uncle Zumo amesema kwa sasa bado hajafikiria kuongeza mke licha ya dini kumruhusu kufanya hivyo.
Uncle Zumo amesema yupo kwenye ndoa kwa miaka tisa lakini ni miaka mitatu tu ya hivi karibuni ndio maisha yameaanza kukaaa sawa hivyo kuongeza mke mwingine atakuwa anamkosea mke wake Habiba.
“Unajua tupo kwenye ndoa kwa miaka tisa ambayo ilikuwa ya shida sana baada ya kuwa maarufu hii miaka mitatu mambo ndo yamekuwa mazuri, kuongeza mke mwingine itakuwa ni kumkosea mkee wangu Habiba.
Akizungumzia kuhusu mahusiano ya wasanii amesema kwa mtazamo wake anaona waigizaji wa kike kutoka Bongo Movie wamekuwa wakiwabeba wasanii wa Bongo Fleva, na kuongeza kuwa huenda kuna kitu wanakipata ambacho wengi hawakijui.
Aidha Uncle Zumo amemshukuru Muongozaji wa Tamthilia ya Jua Kali, Lamatah inayorushwa kupitia Dstv, kwa kumpa nafasi ya kuonyesha kipaji chake nje ya uchekeshaji.