The House of Favourite Newspapers

Waliotupwa lupango na DC Makonda ‘sasa kazi tu’!

1

2.Baadhi ya wakazi wa eneo la kijiji cha Nyakasangwe wakishikilia mabango yaliyoandijkwa ujumbe mbele ya Makonda.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wakazi wa eneo la Wazo kijiji cha Nyakasangwe hii leo.
3.Wananchi walokusanyika kwenye mkutano huo kusikiliza Mkuu wao wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.Wananchi waliokusanyika kwenye mkutano huo kusikiliza Mkuu wao wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.
4.Makonda akiendelea kutoa ufafanuzi wa jambo huku pembeni yake akiwa na viongozi wa jeshi la Polisi wa Wailaya ya Kinondoni.Makonda akiendelea kufafanua jambo, huku pembeni yake akiwa na viongozi wa serikali za mtaa pamoja na jeshi la polisi kutoka wilaya ya Kinondoni.
5.Wananchi wakiendelea  kumsikiliza  Makonda.Wananchi wakiendelea kumsikiliza Makonda.
6.Baadhi ya wananchi wakiendelea kushikilia mabango yaliyoandikwa ujumbe.Baadhi ya wananchi wakiendelea kushikilia mabango yaliyoandikwa ujumbe.
7.Mkutano ukiendelea.Mkutano ukiendelea.
8.RPC wa Wilaya ya Kinondoni, Camilius Wambura  kushoto) akisisitiza jambo fulani kwa wananchi hao.RPC wa Wilaya ya Kinondoni, Camilius Wambura (aliyoko mbele) akisisitiza jambo fulani kwa wananchi hao.
9.Baadhi ya wananchi wakiendelea kufuatila mkutano huku usalama ukiwa wa kutosha eneo hilo.Baadhi ya wananchi wakiendelea kufuatilia mkutano, huku usalama ukiwa wa kutosha eneo hilo.

Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuwaweka rumande kwa takribani saa 6 maofisa wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni waliochelewa kuhudhuria kikao cha utatuzi wa migogoro kwenye Kata ya Wazo jana, mapema leo maofisa hao wameonekana kuanza kazi yao kwa kasi baada ya kufika saa mbili kabla ya kikao kuanza.

Akizungumza kwenye kikao cha pili kilichofanyika katika kata ya Wazo kijiji cha Nyakasangwe nje kidogo ya jiji la Dar, baada ya kile cha jana kuahirishwa kutokana na uchelewaji wa maofisa hao, Makonda amesema kuwa hana tatizo na maofisa wake na kuwataka waelewe kuwa alilazimika kufanya hivyo kutokana na kasi yake ya utendaji na kuwasifu kwa kuwa wavumilivu na kuwahi siku ya leo.

Mbali na hayo Makonda amesema kuwa ameunda kamati inayowahusisha wenyeviti saba na wajumbe kumi na mbili wa kata nzima ya Wazo ambao watakuwa na kazi za kutambua ukubwa maeneo yenye migogoro, kutazama uhalali wa umiliki wa maeneo husika na kuwapa hatimiliki waliothibitishwa kuwa ni wamiliki halali wa maeneo hayo.

Aidha Makonda amewatoa hofu wakazi wa maeneo hayo waliofurika kutaka kujua hatma ya viwanja vyao,akisema kuwa anatambua uwepo wa watu wanaomiliki viwanja hivyo kwa njia ya kurithishwa, kupewa kama zawadi na wengine kuuziwa kwa kutumia kanuni za kijiji na kuongeza kuwa bila kujali wananchi wote waliopeleka malalamiko yao watapata haki zao stahiki.

Alifafanua kuwa anatarajia kuimaliza kabisa migogoro hiyo iliyogharimu maisha ya watu saba huku wengine wakipoteza makazi yao na kuwataka wananchi kuwapa ushirikiano wa kutosha wanakamati watakaozunguka kufanya zoezi hilo la uhakiki katika maeneo yao bila kusababisha uvunjifu wowote wa amani.

“Niwambieni ndugu wananchi ninataka nikiamka Januari Mosi mwakani kila mtu awe kwenye eneo lake akifanya shughuli zake bila hofu yoyote, tukifanya hivyo tutaweka historia ya kuwa wilaya ya kwanza kumaliza migogoro ya ardhi kwa njia ya kistaarabu zaidi na wengine wataiga kwetu,” amesema Makonda.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

1 Comment
  1. Rose Maleko says

    Hapa Kazi tu.

Leave A Reply