×

Carlinhos Amtibulia Kaze Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze amesema kuwa kadi nyekundu aliyopewa kiungo wake mshambuliaji Carlos Fernandez ‘Carlinhos’ imetibua mipango yake katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

 

Kiungo huyo fundi mwenye uwezo wa kupiga pasi ndefu katika mchezo uliopita wa FA waliocheza dhidi ya Kengold FC alishindwa kumalizia mechi baada ya kupewa kadi nyekundu kwa kumpiga ngumi mchezaji wa timu pinzani.

Staa huyo kutoka nchini Angola, anatarajiwa kuikosa michezo mitatu kutokana na adhabu hiyo ya kadi nyekundu kwa kuanzia mechi ya kesho dhidi ya Coastal itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaze alisema kuwa kiungo wake huyo alikuwepo kwenye mipango yake mikubwa katika michezo ijayo baada ya afya yake kuimarika.

 

“Carlinhos na mwamuzi waliingia kwenye mtego wa wapinzani, kwani Carlinhos alichezewa vibaya akapaniki akachukua maamuzi hayo aliyoyachukua, lakini kwangu sidhani kama alistahili kadi nyekundu.

 

“Carlinhos ni mchezaji mzuri, alikuwa ameimarika kwenye fitnesi na kiwango chake, kumkosa kwenye michezo ijayo ya ligi na FA siyo kitu kizuri kwa kuwa alikuwa kwenye mipango yangu katika michezo ijayo,” alisema Kaze

STORI NA WILBERT MOLANDI Dar es Salaam

Leave a Comment