
BILIONEA wa Japan, Yusaku Maezawa, amewakaribisha watu wanane kujiunga nae kwa ajili ya safari ya kuutembelea mwezi katika ndege maalum kutoka kampuni ya Elon Musk SpaceX .
“Ninahitaji watu wa matabaka mbalimbali kujiunga nami,”alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, ambako pia alitoa maelezo ya maombi kwa wale wanaotaka kwenda kupitia kiunganishi hiki shared a link to application details.
Amesema atalipia gharama zote za safari hiyo, kwa hiyo wale watakaosafiri naye katika chombo hicho watasafiri bure.
Chombo hicho kinachoitwa DearMoon, kimepangwa kusafiri mwaka 2023 na hii itakuwa safari ya kwanza ya kihistoria kwa chombo hicho kubeba abiria kwa ajili ya kwenda kutalii mwezini.