×

Video: Global Habari Machi 04 – Rais Mwinyi Awaapisha Mawaziri Aliowateua

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dk.Hussein Mwinyi leo Machi 4,2021 amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa hivi karibuni Ikulu Visiwani Zanzibar.

 

Rais Mwinyi amemwapisha Dkt Saada Mkuya Salum, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Omar Said Shaaban kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda huku Nassor Ahmed Mazrui kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

 

Aidha Rais Dk.Mwinyi amemuapisha Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali, ambaye aliteuliwa February 10 mwaka huu ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment