×

Siri ya rayvanny Kumwangukia Kajala Yafichuka!

BAADA ya staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ kumuangukia muigizaji Kajala Masanja kumuomba radhi, siri iliyopo nyuma ya pazia imefichuka!

 

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, usiku wa kuamkia juzi, Rayvanny aliweka picha ya Kajala na kumuomba radhi kwa kitendo chake cha kuvujisha kipande cha video kilichomuonesha yeye akiwa na mtoto wa staa huyo wakifanya mambo ya faragha (kubusiana).

 

 

“Duniani wakati mwingine kuna vitu tunavifanya ambavyo pengine kwa macho yetu ya ujana tunaona ni sahihi lakini tunasahau upande mwingine wa pili ambao ni wazazi wanaoumia kwa namna moja au nyingine.

 

 

“Nichukue nafasi hii kumuomba radhi dada yangu @kajalafrida (Kajala) na kuwaomba radhi wazazi na yeyote ambaye nilimkwaza kwa kuposti video ambayo inawezekana imetafsiriwa vibaya…kwa sababu sisi ni binadamu na kamwe hatuwezi kukamilika,” aliandika Rayvanny.

 

RISASI lilizungumza na chanzo kilicho karibu na Rayvanny ambacho kiliweka wazi kuwa, sababu ya jamaa huyo kufikia hatua hiyo ni baada ya kuona amebanywa kila kona na jela ilikuwa inamhusu.

 

 

“Alikuwa anakwenda kukumbuna na mkono wa sheria na wakubwa wakamshauri kwamba hili hakuna ujanja lazima uombe radhi maana akikomaa, unakwenda jela.

 

 

“Unajua kina Rayvanny ni wajanja sana. Waliangalia ushahidi alionao Kajala kuhusu lile sakata wakaona kabisa hawachomoki hivyo njia pekee ni kuomba radhi ili mambo yaishe,” kilisema chanzo hicho.

 

 

Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, mbali na kubanywa huko kwenye kona za kisheria, Kajala aliweka sharti la kuombwa radhi mtandaoni ndio mambo yaweze kuisha na Rayvanny aahidi kukaa mbali na mwanaye.

 

 

“Kajala alikubali kuombwa radhi lakini alimpa masharti likiwemo la kukaa mbali na mwanaye lakini pia kuomba radhi mtandaoni ambako ndiko sakata hilo lilipoanzia,” kilisema chanzo hicho.

 

 

TUJIKUMBUSHE

Sakata hili lilitokea katikati mwa Februari mwaka huu mara baada ya Rayvanny kuposti kipande cha video kilichomuonesha akifanya mambo ya faragha na Paula.

 

 

Rayvanny alifanya hivyo na kuzua gumzo kama lote mtandaoni wakati ambao Kajala na mpenzi wake, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ pamoja na binti yao Paula walipokuwa Zanzibar kusherehekea Siku ya Wapendanao, Valentine’s Day hivyo kuwatibulia kabisa sherehe hiyo.

 

 

Baada ya hapo, Kajala aliandika bonge la waraka mtandaoni kumlaumu mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa kumtorosha binti yake na kumpeleka Kwa Rayvanny, kumywesha pombe na kufanya matukio hayo yasiyo na staha.

 

 

Kajala alilifikisha suala hilo katika kituo cha polisi cha Oysterbay jijini Dar ambapo ndipo Rayvanny pamoja na uongozi wake ulipofika kwa ajili ya kulizungumza suala hilo na kufikia hatua hiyo iliyofikia sasa, Rayvanny kuomba radhi.

STORI: ERICK EVARIST

Leave a Comment