
KLABU ya Liverpool imetakiwa kumuuza Mohamed Salah ili kupata fedha za kutengeneza kikosi chao upya kama ambavyo walifanya kwa Philippe Coutinho.
Hayo yamesemwa na nguli wa klabu hiyo, Robbie Fowl-er mara baada ya kuwa na ma-tokeo mabaya hivi karibuni.
Liverpool chini ya Kocha Jurgen Klopp imefungwa mechi sita mfululizo huku mchezo wa juzi Jumapili dhidi ya Fulham ukiwa ni wa sita na kuwaweka kwenye nafasi mbaya ya kutofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Fowler ambaye anashika nafasi ya sita kwa wachezaji waliofunga mabao mengi Liverpool, anaamini kuwa huu ni muda sahihi wa kumuuza Salah kama walivyopata pauni 105m kwa kumuuza Coutinho mwaka 2018.
“Sina tatizo na Salah. Ninampenda sana lakini ukweli ni kuwa naamini huu ni muda sahihi wa kumuuza, mpira bado upo kwake.“
Kama tunataka kufanya maamuzi ni vema tukafanya sasa, kama hana furaha wanatakiwa kufanya maamuzi.“Jurgen Klopp ameshaweka wazi kuwa hataki kuwa na mtu ambaye hana furaha klabuni, naamini hii ni nafasi kama ilivyokuwa kwa Philippe Coutinho.
“Klopp aliona kilichotokea kwa Coutinho hakikuwa sawa, yaani tabia zake, hakutaka sumu ivuruge klabu, akaamua mumu-uza.“Hivyo, kama Salah hana furaha ni vema waka-pita njia zilezile, wakimuuza watapata faida kubwa na kuiboresha timu kwa kipindi hiki,” alisema Fowler.
STORI: LIVERPOOL, ENGLAND