×

Namungo Yaivaa Casablanca Kibabe Leo

WAKATI Namungo ikitarajia kucheza mchezo wa kwanza hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca leo, timu hiyo itawakosa wachezaji wawili katika mchezo huo akiwemo Abdulhalim Humud na Steven Sey.

 

Mchezo huo utachezwa leo Jumatano katika Uwanja wa Mohamed V na Namungo ikiwa ugenini ukiwa ni mchezo wa kwanza katika Kundi D.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa Namungo, Hemed Morocco alisema timu iko vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kupambana kwa ajili ya Tanzania.

 

“Ni mechi ya mwanzo kwetu ila tunaocheza nao tunafahamu wana uzoefu mkubwa kuliko sisi hivyo mchezo utakuwa mgumu lakini tutahakikisha tunapambana kwa ajili ya Tanzania.“

 

Tumejiandaa vizuri na nidhamu ni kubwa kwa wachezaji pamoja na morali, lakini tutawakosa wachezaji wawili ambao ni Abdulhalim Humud na Steven Sey lakini ongezeko la Lucas Kikoti, utaongeza kitu kwenye timu.” alisema Morocco.

Leave a Comment