×

Mnada wa Bajaji Kutikisa Dar Jumamosi Hii – Video

KAMPUNI ya SEPCO DEBT COLLECTION AND AUCTIONEERING COMPANY LIMITED inawatangazia mnada wa hadhara. Kwa idhini tuliyopewa na kampuni ya SUNBEAM AUTO, tutakuwa tunafanya mnada kila Jumamosi… na tutanza Jumamosi hii ya Machi 13, 2021 kuanzia saa 4 asubuhi tutauza Bajaji.

 

 

Ukaguzi wa Bajaji hizi utafanyika Alhamisi na Ijumaa kuanzia saa 3:00 asubuhi – 10:00 jioni katika ofisi za SunBeam zilizopo Barabara ya Nyerere karibu na SIDO, Dar es Salaam.

MASHARITI YA MNADA
1. Mnunuzi atakayebahatika kununua mali hizo atalazimika kulipa papo hapo asilimia 25 ya bei itakatokuwa imefikiwa, na asilimia 75 nyingine atalipa ndani ya siku saba kuanzia siku ya mnada na akishindwa kulipa mnada utarusidiwa na pesa aliyolipa awali haitarudiswha.
2. Mnunuzi atalazimika kuondosha Bajaji aliyonunua mara baada ya kukamilisha kulipa malipo yote taslimu.
3. Gharama zote za kutoa Bajaji alizonunua ni za mteja mwenyewe.
4. Bajaji itauzwa kama ilivyo na ukiharibu haitarudishwa
5. Kwa yeyote atakayeharibu mnada hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Kwa mawasiliano zaidi, fika katika ofisi zetu zilizopo RITA Tower,ghorofa ya 11 Posta jijini Dar es Salaaam au piga simu namba 0715683777 au 0716535221 au 0717593890 au 0713076161

Nyote mnakaribiahwa!

Leave a Comment