
Rais mstaafu wa Somalia, Ali Mahdi Muhammad amefariki dunia Jumatano Machi 10 katika Hospitali ya Nairobi, Kenya alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Rais huyo alizaliwa mwaka 1939 na alikuwa rais wa Somalia kwa miaka saba kuanzia mwaka 1991 hadi 1997 akiwa ni rais wa nne wa taifa hilo.