The House of Favourite Newspapers

Azam Yazipigia Hesabu Pointi za Yanga SC

0

UONGOZI wa Klabu ya Azam, umejinasibu kuwa kwenye mpango wa kutumia faida ya matokeo mabaya ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, ili wao wakae juu yao.

 

Mpaka sasa, Azam wapo nyuma ya Yanga kwa tofauti ya pointi tisa ambapo timu zote zimecheza mechi 23.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Tangu mwanzoni mwa msimu huu tuliweka wazi kuwa tuna jambo letu, na hii ni katika kuhakikisha tunajitahidi kumaliza nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi.

 

“Hivyo hatuna presha na mtu aliye nyuma yetu, bali sisi tunamwangalia aliye juu yetu, na kwa sasa Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi, hivyo malengo yetu ni kujitahidi kushinda michezo iliyo mbele yetu ili kupunguza pengo la pointi lililo kati yetu.

 

“Uzuri ni kwamba Yanga nao hawajawa na mwendelezo mzuri na wameangusha pointi nyingi, hivyo ni jukumu letu kulichukulia hilo kama faida na kuwakaribia au hata kuwazidi.”

JOEL THOMAS, Dar

Leave A Reply