×

Mwigulu: Kiongozi wa Nchi Sio Parish Worker

WATANZANIA wametakiwa kuacha kuibua taharuki kwa kuzusha taarifa za uongo ambazo hazina uthibitisho kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria.

 

 

Akinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, Waziri wa Katiba na Sheria , Mwigulu Nchemba ameonya kwamba wote wanaozusha habari hizo watachukuliwa hatua hata baada ya kupita muda mrefu.

 

 

“Kiongozi wa Nchi sio Parish Worker Kanisani wala sio Mzee wa Kanisa kwamba alipangiwa zamu na hakuonekana, Kiongozi wa Nchi sio Mtangazaji wa TV kwamba alikuwa na kipindi ila hakuonekana, Kiongozi wa Nchi sio Kiongozi wa jogging clubs kwamba anatakiwa kuwa tu mtaani kila siku na kurusha selfie.

 

 

“Tuache upuuzi upuuzi hata kama hatuna jambo la kufanya, umeichafua sana Nchi umeshindwa, mmetamani tukwame mmeshindwa, sasa mnaombea mabaya nchi yetu na Kiongozi wa nchi yetu, sheria inapovunjwa hakuna mipaka wala hakuna muda kupita, kwa wanaoropoka zingatieni kifungu cha 89 cha Penal code na 16 cha Cyber Crime, Serikali ipo kazini,” alisema Nchemba.

 

 

Sambamba na Waziri Nchemba, jana Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa pia alitoa wito kwa wanahabari na wananchi kuendelea na utaratibu wa kupata taarifa kupitia vyanzo rasmi vya habari badala ya kufuata habari za uzushi.

Leave a Comment