The House of Favourite Newspapers

Didier Gomes Awaweka Kikao Kizito Mastaa Simba

0

BIG Bosi wa Benchi la Ufundi la Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amefunguka kuwa alifanya mazungumzo na wachezaji wake ikiwa ni mbinu ya kuwaweka sawa kiakili kwa ajili ya kuondoa mawazo waliyokuwa nayo baada ya kutoka sare kwenye mechi iliyopita dhidi ya Prisons.

 

Kocha huyo ameongeza kwamba, alifanya mazungumzo hayo kwa ajili ya kurudisha hali ya utimamu ya nyota wake kabla ya kucheza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh, leo Jumanne.

 

Gomes ameliambia Spoti Xtra, kuwa aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kuwafanya tena mastaa wake warudi katika hali ya upambanaji baada ya kuona hawakuwa sawa baada ya sare na Tanzania Prisons ya bao 1-1.

“Hatukuweza kufurahi baada ya kumaliza mechi yetu na Prisons kwa sababu tulikosa nafasi ya kuchukua pointi tatu tena tukiwa na nafasi ya kuweza kufunga lakini tukakosa.

 

“Baada ya hapo tunatakiwa kurudi kwenye utimamu wetu, tunatakiwa kuwa sawa na ndiyo maana nilifanya mazungumzo na wachezaji kwa ajili ya kuwaondoa kile ambacho kilikuwa akilini mwao kuhusu mechi hiyo iliyopita.“

 

Tulifanya hivyo kwa ajili ya kuwasaulisha na kuwafanya wawe tayari kwa ajili ya mechi hii na Merrikh ili kupambana na kufanya vizuri kama ambavyo tunataka iwe hivyo na tuingize mguu mmoja kwenye hatua ya robo fainali,” alimaliza Gomes

Leave A Reply