×

Luis Miquissone, Zimbwe Wachaguliwa Kikosi Bora Afrika

NYOTA wawili wa Klabu ya Simba, Luis Miquissone na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’, wametajwa katika kikosi bora cha wiki cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambacho kina wachezaji 16 kutoka klabu sita.

 

Jumanne wiki hii Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan ambapo Luis na Zimbwe walihusika kwa kiasi kikubwa katika ushindi huo.Luis akifunga bao moja na kuasisti bao la Chris Mugalu huku Zimbwe yeye akifanikiwa kufunga bao moja.

 

Ushindi huo umeifanya Simba sasa kufikisha pointi 10 na kuongoza msimamo wa Kundi A la michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

SIMBA

Akizungumza na Championi Jumamosi, kuhusu mafanikio hayo meneja wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Haya ni mafanikio makubwa kwetu, mara ya kwanza tulikuwa na Luis peke yake lakini wakati huu tuna ongezeko la mchezaji mmoja, hii inazidi kuonyesha ukubwa wetu na ile ‘next level’ tunayoimaanisha.”

Joel Thomas,Dar es Salaam

Leave a Comment