×

Majaliwa: Siamini, Nahisi Kama JPM Ananipia Simu – Video

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika hali ya masikitiko na majonzi amesema haamini macho yake iwapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefariki dunia kutokana na ukaribu waliokuwa nao wa kushirikiana katika utendaji ili kulipeleka taifa mbele.

 

 

Majaliwa ameyasema hayo leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kabla ya Wabunge kutoa heshima zao za mwisho kwa hayati Rais John Magufuli.

 

 

“Wengi tulitamani Dk John Magufuli kuendelea kuwa nae kimwili lakini kifo hakizoeleki na wala hakizuilika. Hatuna budi kukubali mapenzi ya Mungu kuwa alitoa na sasa ametwaa.

 

“Kila ninapoona jeneza la Rais John Magufuli, siamini macho yangu, nahisi kama vile napigiwa simu napewa maagizo na maelekezo, imekuwa siku ngumu sana kwangu.

 

 

“Sina kubwa la kusema, waliotagulia wamesema mengi kuhusu mpendwa wetu. Binafsi napata shida kusema, naona kama vile ananipigia simu, ananipa maagizo, naomba mnivumilie, ni siku ngumu kwetu.

 

 

“Mama yake mzazi yupo kitandani kwa miaka miwili, tumuombee Mungu apate nguvu na aweze kunyanyua kitandani, nae Rais wetu mpendwa alale pema peponi,” Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu.

Leave a Comment