
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli umewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya wananchi wa visiwani humo kuuaga mwili huo leo Machi 23, 2021.

Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi, ndiye atakayeongoza maelfu ya wananchi wake kutoa heshima za mwisho kwa shujaa huyu wa Afrika.

Maelfu na maelfu ya wananchi pamoja na viongozi mbalimbali tayari wameshajaa katika uwanja wa Amaani kwa ajili ya kuaga mwili wa Magufuli.

Rais Magufuli alifariki dunia jioni ya Jumatano, Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu kwa maradhi ya moyo.

Aidha, mwili wa Rais Magufuli unatarajiwa kuzikwa Ijumaa, Machi 26, 2021 nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

