
TAMBAZA AUCTION MART & GENERAL BROKERS LIMITED kwa idhini tuliyopewa na Kampuni ya IMARISHA MAISHA FINANCIAL SERVICE LIMITED tunawatangazia mnada wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii ya Aprili 17, 2021 kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Tutauza magari ya wadaiwa walioshindwa kulipa madeni yao, ambapo mnada huo utafanyika katika Ofisi zetu za TAMBAZA zilizopo Sinza Mori, mkabala Kituo cha Mafuta cha Big Born Petrol au karibu na La Chaz Pub. Unaruhusiwa kuja kukagua magari siku tatu kabla ya mnada kufanyika.

MASHARITI YA MNADA
- Mnunuzi atakayebahatika kununua mali hizo atalazimika kulipa papo hapo asilimia 25 ya bei itakatokuwa imefikiwa, na asilimia 75 nyingine atalipa ndani ya siku 14 kuanzia siku ya mnada na akishindwa kulipa mnada utarusidiwa na pesa aliyolipa awali haitarudiswha.
- Mnunuzi atalazimika kuondoa gari/magari yako uliyonunua mara baada ya kukamilisha kulipa malipo yote taslimu vinginevyo utalazimika kulipia storage kwa kampuni ya Tambaza.
- Gharama za kutoa gari alilonunua ni za mteja mwenyewe.
- Gari itauzwa kama ilivyo na ukiharibu haitarudishwa
- Kwa yeyote atakayeharibu mnada hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Kwa mawasiliano zaidi, fika katika ofisi zetu zilizopo Sinza Mori opposite na Big Born Petrol Station au karibu na La Chaz Pub jijini Dar es Salaaam au piga simu namba 0713327989 au 0719 719 346 au 0222701248 au baruapepe [email protected]
Nyote mnakaribiahwa!