×

Kikwete: Sina Shaka na Rais Samia, Ataendeleza Kazi ya Magufuli – Video

 

RAIS mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema ana imani Rais mpya Mama Samia Suluhu Hassan kwani ni mtu sahihi na ataendeleza kazi aliyoiacha mtangulizi wake Hayati John Magufuli.

 

 

Amesema viongozi wastaafu wapo tayari kumpa kila aina ya ushirikiano endapo atahitaji msaada Kikwete aliyekuwa rais mwaka 2005 hadi 2015 ameeleza hayo leo Ijumaa Machi 26, 2021 katika ibada ya mazishi ya Magufuli inayofanyika wilayani Chato Mkoa wa Geita.

 

“Baada ya matatizo ya Zanzibar Rais Mkapa aliunda timu niliyoiongoza Mimi, alikuwepo Dkt. Shein alikuwepo na Samia, nimekufahamu zaidi Rais Samia ulipokuja kuwa Waziri wangu katika Serikali, ulisaidia kuimarisha Muungano kwa kushughulikia kero za Muungano.

 

“Rais Samia hatua zako ni nzuri sana, umetufariji Watanzania, umetufuta machozi na muhimu zaidi umetuhakikishia kuwa nchi ipo katika mikono salama na hakuna litakalo haribika, binafsi sina shaka na uongozi wako kwani nakufahamu kwa muda mrefu.

 

“Kama ulifanikisha vile kwa kiasi kile ulipokuwa Waziri, tunatarajia ufanye makubwa zaidi sasa wewe ndio Rais. Muungano utaimarika zaidi. Kipaji chako cha uongozi kilionekana zaidi na kujipambanua ulipokuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

 

 

“Sina shaka na uongozi wako Mhe Samia nakufahamu vyema katika uchapa kazi na umekuwa waziri kwenye uongozi wangu ukiwa ukishughulikia masuala ya Muungano, ulifanya mambo makubwa na hivyo tunakuamini na kukutegemea zaidi kwenye Urais.

 

 

“Nchi yetu iko katika mikono salama, na hakuna litakaloharibika, binafsi sina shaka na uongozi wa Rais Samia. Wewe ni mbobevu kabisa, Mimi na wenzangu tutakuwa pamoja na wewe, tutume tutaitika, usipotutuma tutaendelea na shughuli zetu.

 

 

“Mimi na wastaafu wenzangu tutakuwa pamoja na wewe, tutume tutakuitika usipotutuma tutaendelea na shughuli zetu,” amesema Kikwete.

 

 

Akizungumzia hotuba ya Rais Samia baada ya kuapishwa Kikwete amesema imewafariji na kuwafuta machozi Watanzania.

Leave a Comment