×

Breaking: Mkurugenzi TPA Akamtwa na TAKUKURU

TAKUKURU inamshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko aliyesimamishwa kazi na Rais Samia Suluhu Hassan kwa tuhuma za ubadhirifu wa TZS bilioni 3.6. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha.

 

 

“Kumshikilia mtu ni suala la kawaida kama kuna tatizo limetokea na kama mlivyomsikia Mhe. Rais amemsimamisha kazi kwa sababu ya matatizo na sisi ni kweli tunamshikilia ili tuweze kufanya uchunguzi vizuri,” amesema Mbungo.

 

 

Taarifa zinaeleza mmemshikilia akiwa anatoroka ni kweli?

“Hapana sisi hatuna huo ukweli wa kutoroka lakini tumemshikilia kwa sababu ambazo isingekuwa vyema mimi niziongee hapa sasa hivi, lakini ni utaratibu tu wa uchunguzi.” amesema Mbungo.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema baada ya upekuzi nyumbani kwake wamemkuta na fedha kiasi cha dola elfu tatu za Kimarekani na fedha za Kitanzania Tsh. Milioni 1.5.

 

 

“Taarifa za Kakoko kukutwa na pesa nyingi ambazo picha na video zake zinasambaa sio kweli, sio za kwake, ni Watu nadhani ni Maadui zake wanajaribu kutengeza hoja ya kuonesha alikuwa na hizo fedha, yeye tumemkuta na USD Elfu 3 na fedha za Tanzania Tsh Milion 1.5,” amesema Mbungo.

 

Leave a Comment