×

Virafanga 185 vya Kobe Vayakamatwa Vikisafirishwa

Maafisa wa forodha nchini Ecuador wamepeta watoto 185 wa kobe waliokuwa wamefichwa ndani ya begi lililokuwa likisafirishwa kutola visiwa vya Galápagos hadi bara siku ya Jumapili.

 

Kobe hao waliokuwa wamefungwa kwenye mifuko ya plastiki walipatikana wakati wa ukaguzi wa mara kwa mara katika uwanja mkuu wa ndege wa visiwa vya Baltra.

 

 

Kumi kati ya kobe hao walikuwa wamekufa, maafisa walisema. Moja ya tisho kubwa inayowakabili kobe wa Galápagos ni biashara haramu ya wanyama katika soko za kigeni.

 

Kobe walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Baltra wanaaminiwa kuwa chini ya miezi mitatu. Maafisa wanaokabiliana na bishara haramu ya wanyamapori wanasema kobe hao wanagharimu zaidi ya dola 5,000 sawa na (£3,600) kila mmoja.

 

 

Inaaminiwa wafanyabiashara walikuwa wamewafunga kwa kutumia plastiki ili wasitambuliwe lakini waendeshaji mitambo ya picha za X-ray katika uwanja wa ndege wagundua kuna kitu ambacho sio cha kawaida.

Leave a Comment