×

Rais Samia Akutana na Rais Obasanjo wa Nigeria

Rais Samia Suluhu Hassan, leo amekutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo katika ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya Hayati Dkt. John Magufuli na Hayati Benjamin Mkapa na kumpongeza Rais Samia kwa kupokea madaraka ya kuwa Rais wa Tanzania.


Pia wamezungumzia hali ya usalama barani Afrika na umuhimu wa wakuu wa nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro mbalimbali inayolikabili Bara la Afrika ambayo imekuwa ikisababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto.


Wawili hao wamezungumzia pia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

 

Leave a Comment