×

CAG: Kigwangalla Kill Challenge Mil 172 Hazikuwa Kwenye Bajeti

 

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonyesha Waziri ya Maliasili na Utalii aliziagiza Hifadhi za Taifa za Ngorongoro na Tanapa kulipa shilingi milioni 172 kwa ajili ya kugharamia shindano la Kigwangala Kill Challenge kuhamasisha wasanii kupanda mlima Kilimanjaro bila kuwepo kwenye bajeti.

 

 

Akitoa ripoti hiyo CAG, Charles Kichere amesema kuwa utaratibu huo ulikuwa nje ya bajeti ya taasisi hizo na hakukuwa na risiti za malipo na hivyo kusababisha hasara kwa Serikali.

 

 

Taarifa ya CAG inaeleza kuwa kulikuwa na maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii kuelekeza malipo kwa Kampuni ya Wasafi, baada ya mahojiano Waziri alisema, kampuni ya Wasafi iliomba zabuni.

 

 

Amefafanua kuwa shilingi milioni 140 zilizolipwa hazikuendana na sheria za matumizi ya fedha za umma.

 

 

“Wizara ililipa milioni 140 kwa kampuni ya Wasafi kwaajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita, hata hivyo hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa baina ya wizara na kampuni ya Wasafi na kushindwa kuhakiki wigo na huduma iliyotolewa na kampuni ya Wasafi,” amesema Kichere.

 

 

Pia, CAG amesema Kaimu Katibu Wizara ya Utalii aliagiza Mamlaka ya Ngorongoro na Wakala wa Misitu (TFS) kulipia matumizi ya Ofisi ya Waziri ambapo Ngorongoro walitoa Milioni 92 na TFS Milioni 55.95.

 

Leave a Comment