
WAZIRI wa Afya wa Austria, Rudolf Anschober ametangaza kuachia wadhifa huo huku akibainisha kuwa sababu kuu ya kuamua kufanya hivyo ni ya uchovu.
Waziri huyo ambaye amedumu kwa kipindi cha miezi 15 tu amesema miezi hiyo aliyokuwa ofisini ameiona kama miaka 15.
Anschober (60) ambaye aliyeteuliwa Januari mwaka 2020 na kuongoza Taifa hilo katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona amesema Taifa linahitaji waziri wa Afya ambaye yupo imara kwa asilimia 100.
Amesema amekuwa akifanya kazi kupitiliza na amechoka, pia amekuwa na changamoto kadhaa za kiafya ikiwemo Shinikizo la Damu.