×

Nape Acharuka: Mwacheni Mama Aandike Kitabu Chake Mwenyewe – Video

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema kwa mujibu wa nyaraka za chama hicho tawala, kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu.

 

 

Nape ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 15, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na taasisi zake kwa mwaka 2021/22.

 

 

Amesema Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri na kutaka wananchi kumpa ushirikiano, “mzee Mwinyi (Ali Hassan- rais wa awamu ya pili) alituambia kila zama na kitabu chake.”

 

 

Amebainisha kuwa wamekuwa na vitabu vitano akirejea marais watano Julius Nyerere, Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli akisisitiza kuwa wito wake kwa viongozi, wabunge wenzake, wanachama wa CCM pamoja na Watanzania kumsaidia Samia kwa kumuunga mkono aandike kitabu cha awamu ya sita.

 

 

“Mhe. Naibu Spika kwenye Document zetu, tumesema kujikosoa na kukosoana ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na sio dalili ya udhaifu. Tusigombane bila sababu Tanzania ni yetu sote tumsaidie mama naye aandike kitabu chake tusimshike mkono kumwandikia kitabu tumwache aandike kitabu chake.

 

 

“Hasa ile inayofanywa na mtu kama Magufuli itajitetea na kujisimamia miaka labda kama mtu ana mashaka na legacy yake lakini kama hamna mashaka na legacy yake itasikilizwa, itaongewa sisi watoto wajukuu na vitukuu kwa sababu haya waliyoyafanya watayakuta tu.

 

 

“Ndugu zangu legacy (alama) haitetewi legacy inajitetea yenyewe hasa ile inayofanywa na mtu kama Magufuli, legacy yake itajitetea, itajisimamia kwa miaka, unless mtu ana mashaka na legacy yake.,” amesema.

 

 

Amesema sasa hivi hawana sababu ya kugombana na hawana sababu ya kutoana macho. “Mimi nimekuwa kiongozi katika chama, nimesimamia idara ya maktaba na nyaraka duniani hakuna chama bora kilicho document vya kutosha CCM ni karibia namba moja kwa kila kitu,” amesema.

 

 

Amesema kwenye nyaraka zao wamesema kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na sio dalili ya udhaifu.

 

Leave a Comment