



MAOFISA usambazaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd ambao ni wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Amani, Risasi na Ijumaa leo wamegawa nailoni maalim kwa ajili ya kufunikia magazeti wakati wa mvua kwa baadhi ya wauzaji wa magazeti jijini Dar es Salaam.
Maofisa hao ambao wamefanya zoezi hilo la kugawa nailon hizo waliongozwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko, Anthony Adam ambao wameweza kuzunguka maeneo tofauti jijini kwa ajili ya utoaji wa nailoni hizo.
Lengo la kugawa nailoni hizo ni kuwawezesha wauzaji wa magazeti kuuza hata kipindi mvua kutokana na msimu wa mvua za vuli zinazoendelea nchini.