
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo amewasilisha kwa njia ya barua hoja binafsi kwa Spika Job Ndugai ili kujadili mfumo wa elimu nchini ambao kwa kiasi kikubwa umejikita kwenye nadharia.
Shigongo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, amesema hayo leo Jumatatu, Aprili 19, 2021, wakati akifanya mahojiano maalum na Global Radio na Global TV Online.
“Elimu yetu inamfanya mtoto kukariri tu na si kumjengea ufahamu waa kutatua changamoto. Nimeongea na Spika Job Ndugai, ninataka kupeleka hoja binafsi Bungeni ili bunge letu lipitie na kujadili mfumo wetu wa elimu nchini, nimekubaliwa na ameniambia niandike barua.
“Tatizo la elimu yetu mtoto anafundishwa ili akumbuke na mtihani na si kufundishwa ili awe na maarifa ya kutatua changamoto. Hakuna practical, field miezi miwili, hujifunzi chochote. Kuna haja sasa ya kuupitia upya mtaala wetu, practical iwe zaidi ya theory.
“Napingana na baadhi ya wabunge ambao wanataka kuwaaminisha watu kuwa kuishia la Saba inatosha, Elimu ni kitu cha muhimu sana, mimi niliishia la saba lakini leo hii nina Degree kwa sababu nathamini Elimu,” amesema Shigongo.