
Ma’Khia Bryant amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Polisi wa Colombus, Jimbo la Ohio kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alishika kisu kuwadhuru Wasichana wengine.
Ma’Khia (16) amepigwa risasi nne kwa milio iliyosikika kwenye video inayomuonesha Msichana huyo akiwa na kisu. Hata hivyo, tukio lililokuwa likiendelea halipo dhahiri.
Polisi aliyefanya tukio hilo ni Nicholas Reardon ambaye aliajiriwa mwaka 2019.