Mjumbe wa NEC Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) kilichofanyika leo Aprili 29, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma.
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM leo Aprili 29, 2021 wamefanya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Jijini Dodoma, kwa ajili ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM unaotarajiwa kufanyika kesho Aprili 30, 2021.
Wajumbe 1876 wa mkutano mkuu maalumu wa CCM wanatarajiwa kupiga kura jina moja litakalowasilishwa katika mkutano huo kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho tawala nchini.
Mkutano huo unafanyika baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kufariki dunia Machi 17,2021 na atakayechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya ni Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho baada ya kifo cha Magufuli, mchakato wa kumpata mwenyekiti mwingine ziliendelea kufanyika na kesho ndio unafanyika uchaguzi huo.
Wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM, wakiwa kwenye Kikao.Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika kikao hicho.Wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM, wakiwa wamesimama kwa muda wa Dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akitii jambo kutoka kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Rais Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM.Wajumbe mbalimbali wa NEC wakiwa katika Kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma.Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman, mara baada ya kumalizika kwa kikao