The House of Favourite Newspapers

Flavour Mkali wa mauno, nyimbo za asili

flevaMwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’.

WAKATI wanamuziki Bongo wakiendelea kuiga wanamuziki kutoka nje na kusahau kabisa muziki wao wa asili, wasanii wa Nigeria wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuimba nyimbo zenye vionjo vya ngoma zao za asili huku mwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’ akiongoza kwenye listi hiyo.

Mwimbaji huyu mwenye ‘body’ la kutosha,anatajwa kupenda kufanya muziki wa asili ya makabila mbalimbali ya Nigeria kupitia baadhi ya nyimbo zake kama vile Nwa Baby, Adamma, Ololufe, Uyi, Ada Ada na nyingine nyingi.

Flavour anajulikana sana Bongo kupitia wimbo wake wa Ashawo ambao ulimpa umaarufu mkubwa kabla ya Wimbo wa Nana alioshirikishwa na Msanii Diamond Platnumz huku staili yake ya kucheza kifua wazi kwa kukata mauno ikimtofautisha na wasanii wengi wa levo yake.

Comments are closed.