×

India Yapokea Msaada Kukabiliana Covid -19

TAIFA la India limeendelea kupokea msaada wa kimataifa ili kukabiana na uhaba wa Oksjeni wakati idadi ya vifo vya virusi vya corona ikiongezeka na kufikia rekodi mpya, katika taifa hilo la Asia Kusini.

 

India imeutanua mpango wake wa utoaji chanjo kwa watu wazima, lakini majimbo mengi yanakabiliwa na uhaba wa dozi licha ya zuio la kuuza nje ya nchi chanjo zinazotengenezwa nchini humo.

 

Kuongezeka kwa idadi ya vifo kumetokea wakati vifaa vya matibabu kutoka nchi za kigeni ikiwemo viwanda vya kuhamishika vya kutengeneza oksijeni  vikisafirishwa katika mji mkuu New Delhi kama sehemu ya juhudi kubwa za kimataifa.

 

Leave a Comment