
BEKI kisiki na mfungaji wa bao lililoipa Simba pointi moja dhidi ya Yanga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Joash Onyango raia wa Kenya, ana hamu kubwa ya kukutana na Yanga wikiendi hii.
Mkenya huyo ambaye alifunga bao la kichwa kwenye sare ya 1-1, hamu yake hiyo imekuja zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kukutana na Yanga ambapo amepanga kuiongoza vema safu yake ya ulinzi isifanye makosa ambayo yatawagharimu.
Ikumbukwe kuwa, Onyango ambaye alikuja kusawazisha makosa yake kwa kufunga bao, ndiye alisababisha penalti kwa kumuangusha Tuisila Kisinda, kisha Michael Sarpong akaenda kufunga bao la kuongoza.Taarifa zinadai kwamba, Onyango alimuomba kocha wake ampumzishe asicheze dhidi ya Dodoma Jiji ili kuwavutia kasi Yanga.

Baada ya kuwakosa Dodoma Jiji ambapo Simba ilishinda 3-1 kwenye Ligi Kuu Bara, beki huyo akaibukia kwenye mechi ya FA dhidi ya Kagera na Simba kushinda 2-1.
Mtoa taarifa alisema: “Kabla ya mechi yetu na Dodoma Jiji, Onyango alimfuata kocha na kumuomba ampumzishe kutokana na kucheza michezo mingi, jambo ambalo kocha alilipokea.
“Mechi iliyofuata dhidi ya Kagera akampa tena nafasi ikiwa ni kama sehemu ya maandalizi maandalizi ya kuivaa Yanga.“Yeye mwenyewe ameonekana kuwa na hamu sana na Yanga akisema anataka kufuta kabisa makosa.
MUSA MATEJA, Dar