
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 9, 2021 amemkabidhi mfano wa funguo ya nyumba Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete kama ishara ya kumkabidhi nyumba mpya ya kuishi iliyopo Wilayani Kinondoni Mkoani Dar es Salaam ambayo amejengewa na Serikali kwa mujibu wa sheria.


