×

Mkurugenzi Mbozi akana kutishiswa kuuawa

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Damas Sutta

 

 

NA MWANDISHI WETU

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe, Hanji Godigodi amekanusha madai ya kutishiwa kuuawa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Songwe, Ellynico Mkola na kuwataka watanzania kupuuza taarifa hizo.

Pia amekana kuona nyaraka za malipo ya Sh milioni 18 ambazo zinadaiwa na Mwenyekiti huyo wa CCM Halmashauri ya Mbozi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Ndolezi.

Kauli hiyo ya mkurugenzi imekuja siku chache baada ya kuzungumza na vyombo vya habari na kudai kuwa ametishiwa maisha na Mwenyekiti huyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe, Hanji Godigodi

 

 

Pia katika taarifa hiyo ambayo vyombo mbalimbali vya habari vilisambaza video za mkurugenzi huyo, zilimuonesha akidai kuwa mbali na kupewa vitisho hivyo, nusura avamiwe na majambazi ambao walikosea nyumba wakaenda kwenye nyumba ya jirani yake.

Akizungumza na waandishi wa habari wilyani Mbozi leo Mei 9, 2021, Mkurugenzi huyo alisema “Mimi nimeona tu mitandaoni Mwenyekiti akionyesha nyaraka madai yake alizonazo ila ofisini yangu haina”

Kutokana na madai hayo, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Damas Sutta akizungumzia kuhusu sakata hilo la nyaraka za ujenzi wa zahanati ya Ndolezi, alisema tayar wamezipata.

Mwenyekiti wa Mkoa wa Songwe, Ellynico Mkola

 

Akizungumza na Global, Sutta alisema “Takukuru wamefanikiwa kuzipata nyaraka zilizosainiwa na Mkurugenzi Hanji Godigodi zikionyesha Rahabu Mkolla anastahili kulipwa na Halmashauri ya Mbozi ilichukua vifaa vya ujenzi toka dukani kwa Mkola kwenda Zahanati ya Ndolezi,” alisema.

Alisema baada ya kukamilisha uchunguzi wa nyaraka hizo watatoa taarifa kwa umma ili kumaliza utata suala hilo.

 

Leave a Comment