
NABII, Mashimo amesema kuwa anaweza kuzuia magoli ya Simba mbele ya Yanga, amesema kuwa hayajui majina ya wachezaji, ameomba kuwa msemaji wa Yanga kwa muda mfupi.
Aidha, Mashimo ameishauri Klabu ya Yanga endapo mechi itapangwa kurudiwa basi wakomae ipangwe mwishoni mwa ligi, hilo litawasaidia Yanga kuifunga bao nyingi Simba.
Mashimo amedai kuwa kuahirishwa kwa mechi hiyo ni shinikizo la baadhi ya watu wa ‘juu’ ambao amedai kuwa ni mashabiki wa Simba huku akidai kuwa alioneshwa katika ulimwengu wa kiroho kuwa walishauriwa na mganga.