
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atawaapisha Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Taasisi Jumatano Mei 19, saa 4:00 asubuhi badala ya Jumanne 18 iliyotangazwa awali.
Aidha Rais Samia atawaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama kuu siku ya Jumatatu Mei 17, 2021 kuanzia saa 9:00 Alasiri.
Viongozi hao wataapishwa kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam.
