The House of Favourite Newspapers

Kipigo cha Simba 4-0, Sauzi Chawaibua ‘Wabunge wa Yanga’

0

BAADHI ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni mashabiki wa Klabu ya Yanga wameendeleza utani wa jadi kwa Klabu ya Simba kwa kuonyesha ishara ya vidole vinne baada ya Timu ya Simba QUEEN kutambulishwa Bungeni jijini Dodoma, leo Jumatatu, Mei 17, 2021.

 

Simba Queen wametambulishwa ikiwa ni siku moja baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Soka la Wanawake Tanzania jana Jumapili.

Ikumbukwe kuwa, juzi Jumamosi, Timu ya Simba (ya wanaume) ilifungwa na Timu ya Kaizer Chiefs bao 4-0 katika mchezo wao wa kwanza wa Robo Fainali ya Mabingwa Barani Afrika.

Leave A Reply