×

Mafunzo ya Ujasiriamali Buchosa Yazidi Kuwapa Nguvu Mpya Wananchi

ZAIDI ya wakazi 200 kutoka kata ya Kalebezo wamehudhuria mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa bure na Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo kwa kushirikiana na Taasisi ya Mjasiriamali Kwanza chini ya Mwalimu mahiri Dkt. Didas Lunyungu ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi wananchi wa jimbo hilo.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwainua wananchi kiuchumi.

Akizungumza na wananchi wakiojitokeza kupata mafunzo hayo yaliyofanyika katika kanisa la EAGT Kalebezo, Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Kesi Msalaba amempongeza Mhe. Shigongo kwa kuona umuhimu wa kuwaelimisha wananchi kiuchumi na kutekeleza ilani ya chama hicho kwa vitendo.

“Tunampongeza Mbunge wetu Mhe. Eric Shigongo kwa uamuzi wake wa kutoa elimu ya uchumi bure kwa wananchi wake wa jimbo zima la Buchosa.

“Na huu ndio utekelezaji mzuri wa ilani ya chama chetu kwa kweli tunampongeza na tunamuombea kwa Mungu aendelee na kazi nzuri hii ya kuleta maendeleo katika Jimbo letu la Buchosa,” amesema Msalaba.

 

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment