×

Don Jazzy Amtetea Mondi “Tajiri Kuliko Walichosema Forbes”


CEO wa Label ya #MavinRecords Don Jazzy kutokea nchini Nigeria anaungana na Diamond Platnumz kuwalaani Forbes kwa orodha yao walioitoa hivi karibuni ya Mastaa wenye Mkwanja Mrefu zaidi Afrika.

 

Kupitia ukurasa wa instagram wa Mondi jana aliwatolea uvivu jarida hilo la Forbes kwa kuchapisha ujumbe ulioashiria kutoridhishwa na list iliyoripotiwa hivi karibuni na vyombo vya habari mbalimbali vikilihusisha jarida hilo.

 

Hivyo #Donjazzy kupitia Post hiyo ame-comment maneno yalioashiria kuungana na staa Diamond Platnumz katika kuwakemea Forbes.

 

“Tell them Baba lao” ✍️….@donjazzy

“He is difinitely richer than that” ✍️…@donjazzy.

 

Pia, mastaa kibao kama vile @thisiswurld @officialpraiz na wengine wameonesha kumuunga mkono staa huyu kwenye post hiyo.

Leave a Comment