×

Kasesela: Sijazindua kiwanda cha Kutengeneza ‘Sehemu za Siri’

MKUU wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amekanusha taarifa za yeye kuzindua kiwanda cha kutengeneza sehemu za siri za mfano.

 

Kasesela amesema; “Nimeona article ya uongo ikisambaa kwenye mtandao ikionyesha nazindua kiwanda cha kutengeneza sehemu za Siri za mfano “dildo” za mwanaume, napenda kukanusha habari hizi sio za kweli.

 

“Hiyo picha ilichukuliwa katika mafunzo ya kupambana na UKIMWI miaka minne iliyopita Chuo Kikuu Mkwawa, Msambazaji alikuwa na nia ovu tu juu yangu, nimemwagiza Mwanasheria wangu analifanyia kazi jambo hili.”

Leave a Comment