
HATIMAYE Jarida maridhawa la siku 100 za Mbunge wa Jimbo Buchosa, Mhe. Eric Shigongo limewafikia wananchi wa kisiwa cha Kome jimboni humo.

Katika kuhakikisha kazi inayofanywa na Mhe. Shigongo katika Jimbo la Buchosa, wananchi wanafahamishwa kwa Kila hatua ambapo Shigongo aliamua kuweka utaratibu wa kuchapisha jarida la kila baada ya miezi mitatu.

Jarida hilo linaonesha kazi zilizofanya gharama zake na kazi zinazotarajia kufanyika katika Kila kitongoji, Kijiji na kata zote za Jimbo hilo.

Jana Jumapili, timu ya Ofisi ya Mbunge Jimbo hilo wakiwa kwenye Kivuko cha Mv. Kome pamoja Mhe. Shigongo akielekea kwenye kutoa semina kwa wajasiriamali kisiwani humo wamewapatia jarida la siku 100 za Shigongo Jimbo Buchosa ambapo watu wengi ambao wamesoma kazi kubwa iliyofanyika kwa muda mfupi wampongeza Mbunge Shigongo.

“Aendelee kuonesha kila kazi inayofanyika ili watu waelewe kwani tangu Jimbo letu lianze haijawahi kupata kiongozi ambaye anaonesha mambo aliyoyafanya kwa vitendo na yanaonekana wazi kwa wananchi wake lakini Shigongo ameliweza huyu ndio kiongozi bora kwetu,” alisema Masuka Jumanne, mkazi wa Kome.

Miongoni mwa mambo ambayo Shigongo ameyainisha katika jarida hilo na tayari ameshaanza kuyafanya ni suala la elimu, kugawa nguo na vifaa vya shule kwa wanafunzi, ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu, ujenzi wa zahanati, miundombinu ya barabara, maji na mengine mengi.
